Namna nzige mmoja anavyosababisha baa
Makundi makubwa ya nzige yaliyovamia Afrika Mashariki na kwengineko mapema mwaka huu wanazaliana tena, na ujio wapili wa wadudu hao waharibifu sasa unatishia tena upatikanaji wa chakula na maisha ya watu. Ni uvamizi mkubwa zaidi kwa robo karne iliyopita. Ilikuwaje hali ikawa mbaya hivi?

Nzige wa jangwani kama huyu - aina ya panzi - kawaida hupenda kuishi maisha ya aibu, ya kibinafsi. Anakuwa kutoka yai, kisha nzige mchanga -ajulikanaye kama hopper - na kisha kupevuka mpaka nzige anayeruka.

Lakini mara kwa mara, hupitia ngazi tafauti za mabadiliko, mathalani wakifika eneo la ukijani wanaacha kuishi kwa kujitenga na kuwa kundi la wadudu hatari.
Katika ngazi hii ya kundi, nzige hubadilika rangi na kuwa katika makundi makubwa yanayopaa kwenda safari za mbali.
Makundi hayo yanaweza kuwa makubwa sana. Kundi linaweza mpaka kuwa na nzige bilioni 10 na kutanda kwenye eneo la mamia ya kilomita. Wanaweza kusafiri kilomita 200 kwa siku moja, huku wakitia hofu na woga maisha ya wakaazi wa vijijini kwa kula mazao yao.
Hata kundi la kawaida tu la nzige linaweza kumaliza mazao ya kuwatosha watu 2,500 kwa mwaka, kwa mujibu wa Sirika la Chakula na Kilimo (FAO), chini ya Umoja wa Mataifa (UN).
Baa kubwa la mwisho la nzige kwa Afrika Magharibi lilikuwa 2003-05 na liligharimu mazao ya thamani ya dola bilioni 2.5 kwa mujibu wa UN.
Lakini kulikuwa na makundi ya nzige pia katika miaka ya 1930, 40 na 50. Baadhi yao walitapakaa katika maeneo mbalimbali mpaka kufikia hatua ya kutangazwa kuwa "baa".
Kwa ujumla, FAO inakadiria kuwa nzige huathiri maisha ya mtu mmoja katika kila watu 10 duniani, jambo linalowafanya kuwa wadudu hatari zaidi wanaohama.
Nzige wa jangwani kama huyu - aina ya panzi - kawaida hupenda kuishi maisha ya aibu, ya kibinafsi. Anakuwa kutoka yai, kisha nzige mchanga -ajulikanaye kama hopper - na kisha kupevuka mpaka nzige anayeruka.
Lakini mara kwa mara, hupitia ngazi tafauti za mabadiliko, mathalani wakifika eneo la ukijani wanaacha kuishi kwa kujitenga na kuwa kundi la wadudu hatari.
Katika ngazi hii ya kundi, nzige hubadilika rangi na kuwa katika makundi makubwa yanayopaa kwenda safari za mbali.
Makundi hayo yanaweza kuwa makubwa sana. Kundi linaweza mpaka kuwa na nzige bilioni 10 na kutanda kwenye eneo la mamia ya kilomita. Wanaweza kusafiri kilomita 200 kwa siku moja, huku wakitia hofu na woga maisha ya wakaazi wa vijijini kwa kula mazao yao.
Hata kundi la kawaida tu la nzige linaweza kumaliza mazao ya kuwatosha watu 2,500 kwa mwaka, kwa mujibu wa Sirika la Chakula na Kilimo (FAO), chini ya Umoja wa Mataifa (UN).
Baa kubwa la mwisho la nzige kwa Afrika Magharibi lilikuwa 2003-05 na liligharimu mazao ya thamani ya dola bilioni 2.5 kwa mujibu wa UN.
Lakini kulikuwa na makundi ya nzige pia katika miaka ya 1930, 40 na 50. Baadhi yao walitapakaa katika maeneo mbalimbali mpaka kufikia hatua ya kutangazwa kuwa "baa".
Kwa ujumla, FAO inakadiria kuwa nzige huathiri maisha ya mtu mmoja katika kila watu 10 duniani, jambo linalowafanya kuwa wadudu hatari zaidi wanaohama.
Mwaka | Kupungua | Kuongezeka ama kwisha | Baa |
2019 | 0 | 18 | 0 |
2018 | 0 | 0 | 0 |
2017 | 0 | 0 | 0 |
2016 | 5 | 0 | 0 |
2015 | 2 | 0 | 0 |
2014 | 7 | 0 | 0 |
2013 | 10 | 0 | 0 |
2012 | 9 | 0 | 0 |
2011 | 7 | 0 | 0 |
2010 | 4 | 0 | 0 |
2009 | 5 | 0 | 0 |
2008 | 8 | 0 | 0 |
2007 | 13 | 0 | 0 |
2006 | 1 | 0 | 0 |
2005 | 0 | 20 | 0 |
2004 | 0 | 23 | 0 |
2003 | 5 | 0 | 0 |
2002 | 0 | 0 | 0 |
2001 | 0 | 0 | 0 |
2000 | 2 | 0 | 0 |
1999 | 4 | 0 | 0 |
1998 | 7 | 0 | 0 |
1997 | 12 | 0 | 0 |
1996 | 15 | 0 | 0 |
1995 | 15 | 0 | 0 |
1994 | 13 | 0 | 0 |
1993 | 20 | 0 | 0 |
1992 | 5 | 0 | 0 |
1991 | 0 | 0 | 0 |
1990 | 3 | 0 | 0 |
1989 | 0 | 15 | 0 |
1988 | 0 | 0 | 26 |
1987 | 15 | 0 | 0 |
1986 | 12 | 0 | 0 |
1985 | 2 | 0 | 0 |
1984 | 0 | 0 | 0 |
1983 | 7 | 0 | 0 |
1982 | 5 | 0 | 0 |
1981 | 5 | 0 | 0 |
1980 | 6 | 0 | 0 |
1979 | 0 | 4 | 0 |
1978 | 0 | 15 | 0 |
1977 | 3 | 0 | 0 |
1976 | 9 | 0 | 0 |
1975 | 7 | 0 | 0 |
1974 | 11 | 0 | 0 |
1973 | 7 | 0 | 0 |
1972 | 5 | 0 | 0 |
1971 | 4 | 0 | 0 |
1970 | 7 | 0 | 0 |
1969 | 0 | 11 | 0 |
1968 | 0 | 25 | 0 |
1967 | 7 | 0 | 0 |
1966 | 2 | 0 | 0 |
1965 | 4 | 0 | 0 |
1964 | 6 | 0 | 0 |
1963 | 0 | 10 | 0 |
1962 | 0 | 29 | 0 |
1961 | 0 | 29 | 0 |
1960 | 0 | 0 | 44 |
1959 | 0 | 0 | 47 |
1958 | 0 | 0 | 41 |
1957 | 0 | 0 | 37 |
1956 | 0 | 0 | 35 |
1955 | 0 | 0 | 43 |
1954 | 0 | 0 | 40 |
1953 | 0 | 0 | 43 |
1952 | 0 | 0 | 27 |
1951 | 0 | 41 | 0 |
1950 | 0 | 33 | 0 |
1949 | 9 | 0 | 0 |
1948 | 12 | 0 | 0 |
1947 | 0 | 29 | 0 |
1946 | 0 | 36 | 0 |
1945 | 0 | 0 | 42 |
1944 | 0 | 0 | 47 |
1943 | 0 | 0 | 43 |
1942 | 0 | 0 | 35 |
1941 | 0 | 24 | 0 |
1940 | 0 | 6 | 0 |
1939 | 5 | 0 | 0 |
1938 | 3 | 0 | 0 |
1937 | 6 | 0 | 0 |
1936 | 6 | 0 | 0 |
1935 | 6 | 0 | 0 |
1934 | 0 | 9 | 0 |
1933 | 0 | 18 | 0 |
1932 | 0 | 0 | 27 |
1931 | 0 | 0 | 35 |
1930 | 0 | 0 | 45 |
1929 | 0 | 0 | 41 |
1928 | 0 | 0 | 34 |
1927 | 0 | 22 | 0 |
1926 | 0 | 8 | 0 |
Chanzo: FAO | |||
Muhimu: Kupungua, inamaanisha kuwa nzige wangalipo japo kwa idadi ndogo; kuongezeka inamaanisha mlipuko wa nzige unaoongezeka kwa kuzaliana; baa inamaanisha mtawanyiko mkubwa na wa nguvu kwa zaidi ya mwaka mmoja; mwisho wa wa baa ndiyo kwisha . |
Kundi jipya la nzige linakuwa
Mapema mwaka huu,makundi mabaya zaidi ya nzige kwa miongo kadhaa yalivamia mazao Afrika Mashariki na kwengineko na kutishia usalama wa chakula katika eneo lote hilo.
Wadudu hao waharibifu walisambaa kwa kasi mwezi Januari na Februari kupitia nchi kadhaa za Afrika Mashariki- ikiwemo Kenya,Ethiopia na Somalia. Ulikuwa mlipuko mkubwa zaidi kwa Kenya kwa zaidi ya miaka 70, huku Somalia na Ethiopia miaka 25.
FAO sasa inahofia kipindi cha mvua cha mwezi Machi na kuendelea kitasababisha wimbi la pili la uvamizi wa nzige hao, hali ambayo ni ''tishio'' kwa maisha ya watu katika eneo hilo kwa mara nyengine tena.
Idadi yao huenda ikaongezeka mara 20, inaonya FAO kama juhudi za kuwadhibiti hazitafanyika.
Nchi kadha zipo kwenye hatari ya kuvamiwa na nzige

Hali huenda ikawa mbaya zaidi katika eneo la Afrika Mashariki- ambalo tayari linakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mzozo, ukame na mafuriko. Lakini hali ni ya kutia hofu pia nchini Iran na Yemen,ambako FAO inasema makundi mapya ya nzige hao yanaibukia.
Nzige hao tayari wameshaharibu maelfu ya ekari kote Afrika Mashariki.
Kufikia kilele chao mapema mwaka huu nzige hao walikuwa wanakula tani 1.8 za uoto kwa siku kwa kilomita 350 za mraba, kwa mujibu wa FAO.
FAO wanaamini kuwa kundi moja la nzige nchini Kenya limesambaa kwenye eneo la kilomita 40 kwa 60.
Je nzige wanaweza kula kwa kiasi gani?
Nzige mkubwa anaweza kula gramu 2 kwa siku.
Ujio wa wimbi jipya na kubwa zaidi la nzige nchini Ethiopia na Kenya, ni jambo la kuogopesha, lakini muda pia wa wimbi hilo kurejea ni hatari zaidi anasema KeithCressman,Afisa wa ngazi ya juu wa FAO ambaye ni mtaalamu wa masuala ya nzige.
"Huu ni mwanzo wa msimu wa mvua na katika nchi hizo watu wameanza shughuli za upanzi. Mbegu zimeanza kuota na sasa tuna nzige.''
Nzige waliokomaa sasa wataanza kutaga mayai tayari kwa kizazi kingine ambacho kitakuwa kimekomaa wakati wa mavuno. Bw. Cressman anasema, hali hiyo itakuwa tishio mara mbili kwa maisha ya watu.

Janga la nzige pia linajiri wakati ambapo mataifa yanakabiliana na virusi vya corona pamoja na marufuku yakudhibiti watu kutembea, hali ambayo inatia ugumu katika hatua za mapambano na wadudu hao.
Ali Bila Waqo, 68, ni mkulima kutoka kaskazini mashariki ya Kenya, alikuwa akitegemea mazao mazuri msimu huu, baada ya mvua za hivi karibuni baada ya ukame.
Lakini nzige wameteketeza mahindi na maharage yake yote.
"Wamekula mazao yetu karibu yote, na ambayo hawakula yalinyauka," anasema. "Hii imetuumiza sana. Tumekiona chakula kwa macho yetu, lakini hatukuweza kukifurahia."
Bwana Waqo, ambaye anakumbuka uvamizi mwengine miaka ya 1960, aeleza namna gani nzige hao walivyofanya anga kuwa la giza.
"Kulikuwa kweusi na usingeweza kuliona jua," amesema.
Hali mbaya ya hali ya hewa imesababisha janga hili.
Chanzo cha uvamizi huu kinaanzia kwenye vimbunga na mvua kubwa kwa 2018-19.
Nzige wa jangwani kwa kawaida huishi katika maeneo makavu baina ya nchi 30 kuanzia Afrika Magharibi mpaka India - eneo ambalo lina kilomita za mraba milioni 16.
Hata hivyo, unyevu na hali ya hewa nzuri kwao kwa miaka miwili chini ya Rasi ya Uarabuni ikaruhusu vizazi vitatu vya nzige kutanuka bila kubainika, UN inaeleza.
Nzige hao wamekuwa wakizaliana toka 2018.

Kufikia mwanzoni mwa 2019, makundi ya mwanzo yalihamia Yemen, Saudi Arabia na Iran na kuzaliana zaidi kabla ya kuhamia Afrika Mashariki.
Makundi zaidi yalijitengeneza na kufikia mwishoni mwa 2019 yakaongezeka Eritrea, Djibouti na Kenya .

Kizazi cha nzige wa machipuko kinatarajiwa kuvamia Afrika Mashariki ,Yemen na kusini mwa Iran miezi michache ijayo
Japo uvamizi huo ni mgumu kupambana nao kutokana na eneo kubwa ambalo nzige hao huathiri, Bw Cressman wa FAO anaamini kuwa udhibiti wa awali ungeweza kufanyika.
"Kama kungekuwa na hatua kubwa na za ufanisi za udhibiti katika nchi muhimu, ingeliwezekana kupunguza ukubwa wa hali ya sasa," amesema.
Watu wakijaribu kupambana na makundi makubwa ya nzige
Kwa kuwa makundi ya nzige Afrika Mashariki sasa yana ukubwa usiomithilika na uwezo mkubwa wa uharibifu, nchi zinahangaika kupambana nao.
Kuwazuia kunategemea mambo makuu mawili - uangalizi na njia sahihi za udhibiti .
Kituo cha Taarifa cha Nzige wa Jangani, ambacho kinaendeshwa na FAO, kinatoa taarifa za utabiri, onyo la awali, muda, ukubwa na eneo la uvamizi na kuzaliana.
Lakini idadi ya nzige inapofikia kiwango hatarishi, kama hali ilivyo kwa Pembe ya Afrika, hatua za haraka hutakiwa kuchukuliwa ili kupunguza idadi, pamoja na kuzuia makundi kujikusanya na kusambaa.
Jinsi gani makundi ya nzige hudhibitiwa

Japo kwa sasa hakuna utafiti juu ya suluhisho bora zaidi la kimazingira, kama dawa za kibailojia ama wadudu wanaoshambulia nzige, njia ya kawaida zaidi ya udhibiti inayotumika ni unyunyuziaji wa dawa.
Kuwanyunyizia nzige kupitia pampu za mkono, magari au ndege, makundi hayo yanaweza kuteketezwa kwa kemikali kwa muda mfupi.
Kwa sababu hiyo, FAO kwa sasa inashirikiana na serikali katika kampeni kadhaa za kuwanyunyizia dawa nzige hao kwa kutumia ndege.
Kufikia sasa zaidi ya hekari 240,000 katika nchi 10 zimenyunyuziwa dawa na mamia ya watu wamepewa mafunzo ya jinsi ya kupambana nao.
Kampeini hiyo imefanya vizuri zaidi ikilinganishwa na miaka ya awali,Bw. Cressman anasema hatua ya kutdhibiti menendo ya watu kutokana na virusi vya corona haijaathiri shughuli hizo kwa vyovyote vile

Lakini ni ngumu sana kudhibiti kiasi kikubwa cha nzige hao katika eneo kubwa na la ndani sana. Hauwezi kujua ni asilimia ngapi ya nzige ambao umewafikia, anaelezea Bw. Cressman
Lakini hatua zilizochukuliwa zitaamua nini kitakachofuata baadae. Kama nzige wataendelea kuvuka mipaka zaidi na kuathiri maeneo mengine, na kuharibu mazao zaidi basi uvamizi huo utatangazwa kuwa "baa".
Kutokana na hilo ni muhimu ''kuungana na kushirikianakwa kupeana maarifa kielimu'' ili kuzuia uharibifu zaidi,anaongeza Bw.Cressman.
Lakini kwa mkulima wa Kenya Ali Bila Waqo na familia yake, hatua yoyote kwa sasa itakuwa imeshachelewa. Kitu pekee ambacho waliweza kufanya kudhibiti nzige walipovamia ni kupiga madebe na kelele.
Hata hivyo, bado anakitazama kilichotokea kwa jicho la falsafa.
"Ni mapenzi ya Mungu. Hili ni jeshi lake," anasema.
Utambuzi
Maneno na uzalishaji na Lucy Rodgers, uzalishaji na Joe Inwood, usanifu na Zoe Bartholomew na Millie Wachira, uendelezaji na Becky Rush, Catriona Morrison na Purity Birir. Picha za nzige na Swidbert R Ott na Stephen Rogers na Getty Images. Picha za wakulima Kenya na BBC.