
Majanga huishaje?
Sisi tuko katika mtego wa janga kuliko mwingine katika kumbukumbu ya maisha. Wakati watu wanaweka matumaini yao juu ya chanjo ya kulifuta janga, ukweli ni kwamba maambukizi mengi ambayo mababu zetu wa zamani walikumbana nayo bado tuko nayo.
Shusha chini ↓ kujua namna gani baadhi ya majanga hayo yalikwisha, na kutupa mwanga kuhusu mustakabali wetu

Huyu ni Yasmini
Kama sisi, wazee wake wa zamani walinusurika kwenye majanga kadhaa
Tukurudishe nyuma wakati huo uone walikuwa wakikabiliwa na magonjwa gani.
Katika miaka ya zamani, karibu vizazi 60 vilivyopita, ndugu wa Jasmine waliishi nyakati za milipuko ya ugonjwa wa tauni.
Ugonjwa, ulisababishwa na bakteria waliosambazwa na viroboto vya panya na kupitia matone ya mate kutoka njia ya mfumo wa upumuaji.
Bakteria Yersinia Pestis husambaa miongoni mwa jamii ya panya

Iliwaua mamilioni ya watu katika kipindi cha miaka 2,000.
Maafa ya vifo katika miaka ya 1346-1953 yanatazamwa kuwa mlipuko mbaya zaidi kuwahi kutokea.
Tauni imeua mailioni ya watu zamani, lakini sasa wanakufa wachache.
Inaaminika kuwa ugonjwa, unaosababisha uvimbe na maambukizi ya tezi, ziitwazo buboes, hatimaye ulidhibitiwa kwa watu kuwa karantini na kuimarisha usafi, miongoni mwa mambo mengine.
Lakini hakuna lolote kati ya hayo yangefanyika bila kuelewa namna ugonjwa unavyosambaa, anasema Steven Riley, Profesa wa magonjwa ya kuambukiza kutoka shule ya kitabibu ya Imperial jijini London. Hili ni suala ambalo mpaka sasa linafanya kazi.
'Mara unapokuwa na uelewa, na ukasambaza taarifa tayari unakuwa na uwezo wa kuchukua hatua kupunguza kasi ya maambukizi,''anaeleza.
Bado maambukizi ya tauni yanajitokeza kwa mfano, nchini Mongolia mwezi Julai mwaka huu-na kwa nadharia, Yasmini anaweza kupata maambukizi.
Idadi ya maambukizi hata hivyo iko chini, na ugonjwa unaweza kukabiliwa kwa dawa aina ya antibiotics.
Mamia ya miaka baadae, jamii ya zamani ya Yasmini ilikabiliwa na surua.
Ugonjwa, ulisababishwa na virusi variola minor, ni moja ya virusi hatari kwa binadamu.
Husababisha vipele vyenye maji maji vinavyoota mwili mzima, na karibu watu watatu kati ya kila watu 10 walikufa kutokana na ugonjwa huo.
Unaweza kuambukizwa kwa njia ya matone kutoka kwenye pua au mdomo au vidonda vya mtu aliye na ugonjwa.
Virusi vya Variola minor havitokani na mnyama

Kama ilivyo kwa tauni, surua iliua mamilioni ya watu-milioni 300 karne ya 20 pekee.
Surua iliua karibu watu milioni 350- hakuna sasa anayekufa kwa ugonjwa huo.
Lakini, shukrani kwa chanjo iliyoanzishwa mwaka 1796 na Daktari Muingereza Edward Jenner na jitihada za kisayansi, ugonjwa umemalizwa kabisa, ingawa ilichukua karibu karne mbili kufanya hivyo.
Surua inaendelea kuwa ugonjwa wa binadamu ulioondolewa kwa namna hii. Profesa Riley anatazama hatua hii kama moja ya mafanikio makubwa kuwahi kufikiwa na mwanadamu, ikichuana na mafanikio ya kutua mwezini.
'Inaweza kutazamwa kama malipo makubwa kwa uwekezaji wa Umma uliofanyika,'' anasema, akieleza jinsi dunia ilivyowekeza na kufanikiwa kuoondoa ugonjwa.
Sababu ya mafanikio haya ya kisayansi, sisi, na Yasmini , hatuko hatarini tena.
Kisha, vizazi vinane tu vilivyopita mababu wa mababu wa Yasmini walikabiliwa na kitisho cha ugonjwa wa kichocho.
Ugonjwa, unaosababishwa na kuchafuka kwa chakula au maji ya kunywa, umeua mamilioni ya watu ndani ya majanga saba, kwa mujibu wa WHO.
Vijidudu viitwavyo vibrio cholerae vinapatikana kwenye chakula kilichochafuka au maji

Lakini katika kuboresha usafi katika nchi za Magharibi zimeondosha tishio hilo, na kuathiri zaidi nchi zenye kipato cha nchini na kuua watu kati ya 100,000 na 140,000,kwa mujibu wa WHO.
Kichocho kimeua mamilioni, na maelfu bado wanakufa
'Unajiepusha mwenyewe na kichocho,'' anasema Prof.Riley. ''Ikiwa utakosea kufanya, utasambaa haraka sana.''
Kwasababu ya hili, ikitegemea mahali ambapo Jasmine anapaita nyumbani, anaweza kuwa hatarini kupata ugonjwa na kufa, ingawa kuna chanjo na tiba rahisi dhidi ya ugonjwa huo.
Familia ya Jasmine waliishi kipindi ambacho kulikuwa na majanga kadhaa ya mafua. Kubwa kuwahi kurekodiwa ni mwanzoni mwa karne ya 20, wakati wa mabibi wa mabibi na mababu zake.
Janga la homa ya mafua, wakati mwingine huitwa mafua ta Uhispania, ni moja kati ya milipuko mibaya katika historia ya hivi karibuni na kuua watu milioni 50-100 duniani.
Kama ilivyo kwa virusi vya corona hii leo, kujitenga na kukaa karantini kulipunguza kasi ya maambukizi.
Virusi aina ya H1N1 vilisababisha janga la mafua ya Uhispania

Baada ya awamu mbili kati ya mwaka 1918 na 1920, virusi vya H1N1 viliondoka na kuanza kwa aina nyingine ya mafua yanayojitokeza kila mwaka
Mamilioni walikufa kutokana na mafua ya Uhispania- na mafua ya msimu bado huua
Lakini majanga ya mafua mengine yalifuata.
Mafua ya Hong Kong ya mwaka 1968 yaliua watu milioni moja na pia bado yanasambaa kama mafua ya msimu. Kama inavyofanyika kwa mafua ya nguruwe- aina ya virusi vya H1N1- ambavyo viliathiri karibu asilimia 21 ya watu duniani mwaka 2009.
Mafua yameendelea kuwa ''janga la kutisha'', anasema Prof. Riley, na Jasmine na sisi, tumeendelea kuwa katika hatari ya kupata janga jingine linalosababishwa na virusi hivyo.
Pia tuko hatarini kupata mafua ya msimu, ambayo yanaendelea kuua maelfu kila mwaka.
Kisha, karibu miongo kumi iliyopita,wazazi wa Jasmine waliishi katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI- baadhi wakitambua kama janga, WHO ikiita ''ugnjwa wa kuambukiza''
Virusi vya Ukimwi (HIV) vilisambaa kwa njia ya majimaji yaliyo ndani ya mwili- vimesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 32 duniani mpaka sasa.
Virusi hushambulia mfumo wa kinga wa binadamu

Virusi vya ukimwi vinaweza kutazamwa kama '' vibaya zaidi kuwahi kutokea'', anasema Prof Riley, kwasababu ya urefu wa muda mpaka kuonesha dalili na idadi ya vifo. Husambaa haraka kwasababu watu hawajui kama wana virusi.
Hatahivyo, maendeleo katika hatua za uchunguzi na kampeni duniani-tumebadili tabia zetu zinazohusu masuala ya ngono na ongezeko la matumizi ya sindano salama kwa watumiaji wa dawa za kulevya-ambavyo vimesaidia kupunguza kasi ya maambukizi.
Pamoja na hayo, takribani watu 690,000 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa ukimwi mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za WHO.
Virusi vya ukimwi vimeua mamilioni- na maelfu bado wanakufa
Ingawa hakuna tiba ya virusi vya ukimwi, kama Jasmine aliishi katika nchi yenye huduma bora ya afya na upatikanaji wa dawa za kupunguza makali, angeweza kuishi maisha marefu na kuwa na afya njema.
Hatahivyo, kama aliishi katika nchi zenye kipato kidogo cha kiuchumi na kutopata huduma nzuri, bado angekuwa kwenye hatari.
Miongo miwili mpaka mitatu baadae- wakati Yasmini mwenyewe akiishi-alikutana na tishio la Sars na Mers.
Ugonjwa unaoathiri mfumo wa upumuaji (Severe Acute Respiratory Syndrome- ni ugonjwa hatari wa kwanza uliosababishwa na virusi vya corona- na kuua zaidi ya watu 800 mwaka 2002 na 2003, kwa mujibu wa WHO.
Ugonjwa wa Sars (ufahamikao kama Sars-Cov) ulibainika mwaka 2013

Lakini mpaka mwishoni mwa mwezi Julai mwaka 2003, hakukuwa na ripoti ya maambukizi mapya, na WHO imetangaza mlipuko huo kuisha.
Muda mfupi baadae ugonjwa wa Mers, (Middle East Respiratory Syndrome, ambao pia hutokana na virusi vya corona, uliua watu 912, wengi kutoka Rasi ya Arabuni.
Wakati hatari ya kupata maambukizi ya virusi viitwavyo Mers-Cov, nchini Uingereza kwa mfano, ukionekana kuwa chini sana, hatari imeendelea kuwa juu Mashariki ya Kati-maambukizi yaliyotokana na ngamia.
Sars imeua watu zaidi ya 800
Wakati Yasmini akiwa hatarini kupata Mers, hatari ya maambukizi iko chini katika nchi nyingi.
Sasa, Yasmini na kipindi cha maisha yetu, tunakabiliwa na aina ya ugonjwa mpya wa virusi vya corona, unaoshambulia mfumo wa upumuaji, Covid-19.
Sars-Cov-2, ni aina ya virusi vya Sars vya mwaka 2003 na vinatazamwa na wataalamu kama vya kipekee, kutokana na dalili zake- hatari ya kuua na maambukizi ya hali ya juu ya watu bila kuonesha dalili au kabla ya maambukizi.
'Kwasababu hiyo,watu wengi wameshindwa kuudhibiti,'' alisema Prof Riley.
Virusi vya Sars-Cov-2 vinahusiana na virusi vya Sars vya mwaka 2003

Zaidi ya watu milioni moja wamepoteza maisha, lakini idadi kwa ujumla pengine inaweza kuwa juu zaidi.
Virusi vipya vya corona vimeua watu zaidi ya milioni moja mpaka sasa
Wakati mchakato wa kutafuta chanjo na tiba inayofaa ukiendelea, hatari imeendelea kuwepo kwa watu wengi duniani.Jasmine, kama ilivyo sisi, yuko kwenye hatari.
Ni nini kinachofuata?
Hivyo, virusi vya corona ambavyo sasa vinasambaa kwenye jumuia, ni vya karibuni katika orodha ya majanga yanayosababishwa na virusi au bakteria.
Janga kubwa zaidi limeua mamilioni ya watu

Ongezeko la elimu kuhusu maambukizi, kampeni za kiafya, tiba na chanjo yalikuwa sehemu ya jitihada za kumaliza majanga hayo hapo zamani.
Hatua hizo hizo kwa janga la sasa huenda pia zikasaidia kumaliza janga la virusi vya corona.

Ingawa ''chanjo salama na yenye ufanisi'' inaweza ikawa suluhisho, anasema Prof Riley, ''kuipata hakuna uhakika''
Badala yake, tunaweza kuishi nao huku tukiweka njia za kuepuka maambukizi
'Hakika ndani ya miaka mitano, kuna matumaini, kuwa huenda tukawa na chanjo nzuri ambayo itatumika dunia nzima au tutakuwa tumekusanya kinga ya kutosha na kujifunza namna ya kuishi na milipuko midogo,'' amesema Profesa.
Kama ilivyothibitishwa kuondolewa kwa ugonjwa wa surua, jamii ya kisayansi ikikaa pamoja, matokeo mazuri yanawezekana.
Ingawa virusi vya corona ni changamoto, kwa sababu ya maambukizi ya watu ambao hawana dalili za ugonjwa, Prof Riley anasema anaamini kuwa mchakato wa kuuondosha ugonjwa utafanikiwa.
'Ulimwengu haujawahi kuwa na mradi kama huu hapo kabla,'' alisema ''Nina matumaini utakuwa wa mafanikio kwa kiasi fulani''.
Hatahivyo, ni vizuri kukumbuka kuwa kwa kiasi kikubwa vimelea vya magonjwa ambayo yalikumba dunia awali bado vipo. Wakati janga likiisha, virusi na bakteria wanaosababisha maambukizi -husalia.