Wagombea wakuu wa urais DR Congo
MARTIN FAYULU (MUUNGANO WA LAMUKA)
Muungano wa Lamuka
Alizaliwa Kinshasa 21 Novemba 1956
Ni Mkristo
Anafahamika kama mwanajeshi wa wananchi, aliongoza maandamano dhidi ya Rais Joseph Kabila
Alifanyia kazi Exxon Mobil kwa miaka 20 years, alistaafu 2003 akiwa mkurugenzi mkuu wa afisi ya kampuni hiyo Ethiopia
Alichaguliwa mbunge 2006 na 2011
Alianzisha chama cha Commitment for Citizenship and Development (ECiDé) mwaka 2009
EMMANUEL RAMAZANI SHADARY
Common Front for Congo (FCC)
Alizaliwa 29 Novemba 1960 Kasongo, mashariki mwa DR Congo
Mshirika wa muda mrefu wa Rais Kabila
Aliteuliwa waziri wa mambo ya ndani 2016
Amewekewa vikwazo na EU kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu katika kujaribu kuzima maandamano ya upinzani
Anafahamika kwa ukali wake na kutotetereka, na jina lake la utani ni "make-it-happen" (fanikisha).
FELIX TSHILOMBO TSHISEKEDI
Union for Democracy and Social Progress (UDPS)
Alizaliwa Kinshasa 13 Juni 1963
Lina lake la utani ni Fatshi, ufupisho wa Felix Antoine Tshilombo
Babake alianzisha chama cha UDPS mwaka 1982
Alikwenda Ubelgiji mwaka 1985
Alisomea biashara na utangazaji wa mauzo
Aliteuliwa kiongozi wa UDPS Machi 2018
Ameahidi kupatia kipaumbele vita dhidi ya umaskini