Kampeni yake imejikita kati mafanikio yake kwenye sekta za madini, ujenzi wa miundombinu, elimu bure na mapambano dhidi ya rushwa.
Awamu yake ya kwanza pia imekosolewa kwa ukandamizaji wa haki za binadamu.
Ni mgombea wa chama tawala ambacho kipo madarakani toka uhuru, hivyo anatarajiwa kushinda uchaguzi huu.
Magufuli, 60, alichaguliwa Bungeni mara ya kwanza 1995 na kupata umaarufu akihudumu katika wizara ya ujenzi alipopata jina la utani la tingatinga.
Alimiminiwa risasi na wasiojulikana Setemba 2017, japo amenusurika shambulio hilo limemuacha na majeraha ya kudumu.
Alirejea Tanzania mwezi Julai 2020 baada ya miaka mitatu ya ughaibuni ili kugombea urais kupitia chama kikuu cha upinzani Chadema.
Kampeni yake imejikita kwenye kuheshimu haki za binadamu na kukuza uchumi wa watu.
Mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu alichaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 na 2015 na kuhudumu kama mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
Alituhumiwa ndani ya CCM kuwa alikuwa na mipango ya ‘kumhujumu’ Magufuli kwenye uchaguzi wa ndani ya chama 2020.
Sasa ni mgombea wa ACT, ambacho kimeweza kukua kutoka kuwa chama kidogo mpaka moja ya mihimili ya upinzani kwa kipindi kifupi.
Kachero mstaafu, alihudumu kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya rais mstaafu Jakaya Kikwete toka 2007 mpaka 2015.
Mwanasiasa mwandamizi wa upinzani ambaye amegombea urais katika chaguzi zote kasoro mwaka 2015.
Alikuwa kinara wa upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 na 2005.
Ushawishi wake ndani ya upinzani umepungua baada ya migogoro ya ndani ya CUF iliyolazimisha kundi hasimu kwake kujitoa chamani.
Profesa Lipumba ni moja ya wasomi maarufu wa uchumi nchini Tanzania ambapo alisoma shahada zake za juu kutoka chuo kikuu maarufu cha Stanford, Marekani.