Samia Suluhu Hassan: Maadhimisho ya siku 100 za kwanza za rais wa sita wa Tanzania

Rais Samia Suluhu

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Tanzania.hatua hiyo inafuatia kifo cha ghafla cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli, mwezi Machi mwaka huu. Tarehe 26 mwezi Juni atakuwa ameadhimisha siku 100 ofisini. Hivyobasi tunauliza amepata ufanisi gani katika siku 100 za kwanza tangu achukue madaraka?

Akiwa Rais wa Tanzania , rais Samia Suluhu Hassan anakuwa rais wa tatu wa kike barani Afrika, Hii ni baada ya marais wa zamani Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Joyce Banda wa Malawi.

Kwa sasa Rais wa Ethiopia ni Bi. Sahle -Work Zewde ijapokuwa hana mamlaka

Rais huyo mwenye umri wa miaka 61 kwa mara ya kwanza alichaguliwa kama mwanachama wa bunge la Zanzibar la mwaka 2001. Alipatiwa kiti maalum kilichohifadhiwa wagombea wanawake

Ni machache yanayojulikana kuhusu maisha yake ya kibinafsi. Ameolewa na msomi wa kitengo cha kilimo , Hafidh Ameir, ambaye amekuwa haonekani mara nyingi

Wawili hao hawajawahi kupigwa picha wakiwa pamoja tangu alipokuwa makamu wa rais

Wana watoto wanne , ikiwemo mmoja ambaye kwa sasa ni mwanchama wa bunge la Zanzibar

Kama viongozi wa kike hatubabaiki tunapokumbana na tatizo. Sisi husikiliza kwa makini na kufikiria kabla ya kufanya uamuzi Rais Samia Hassan Suluhu
Raia wa Tanzania akubali kitakasa mikono kutoka kwa msanii wa Tanzania Alex Kalemara kulia, kwa jina maarufu Tanzania Joker, huku akitoa hamasa  kuhusu kuenea kwa maradhi ya Corona . Serikali ya Tanzania imetoa wito kwa wananchi kufuata masharti ta WHO kuhusu Corona. GETTY/ERICKY BONIPHASE - AFP

Kukabiliana na wazo la kutokuwepo kwa Corona

Rais Samia ameanzisha masharti ya kukabiliana na Corona

Pia aliwataka Watanzania kuheshimu masharti ya kukabiliana na mlipuko wa corona. Hatua hiyo ni kinyume na kile ambacho mtangulizi wake rais Magufuli ambaye alikuwa na msimamo mkali kuhusu maradhi hayo kabla ya kubadilika na kuwaruhusu raia kuvalia barakoa zilizotengenezwa nchini humo

Rais Samia akipokea ripoti kuhusu ushauri wa corona kutoka kwa Profesa Said Aboud, mwenyekiti wa kamati ya Corona nchini Tanzania. IKULU YA RAIS TANZANIA

Mwezi Juni 2021, WHO ilitangaza kwamba Tanzania ilianzisha mpango wa kuagiza chanjo kwa raia wake kupitia mpango wa Covax

Msemaji wa serikali ya Tanzania amesema kwamba ataliangazia suala hilo hivi karibuni

Mapema mwezi Juni, serikali ilikuwa imeruhusu kuingizwa kwa chanjo nchini humo kupitia mashirika ya kimataifa na balozi kwa wafanyakazi wake.

Upungufu wa uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa wasiwasi katika uongozi wa Rais Magufuli ambapo  baadhi ya vyombo vya habari , hususan vile vilivyokosoa serikali , vilipigwa marufuku. GETTY/ERICKY BONIPHASE - AFP

Kunyoosha mkono wa diplomasia

Mwezi Aprili Rais Samia aliitaka wizara ya habari kuondoa marufuku dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vimefungiwa kutokana kuikosoa serikali. Serikali hatahivyo baadaye ilibadilisha uamuzi wake ikisema kwamba marufuku hiyo iliondolewa kwa runinga zilizopo mitandaoni na sio vyombo vingine vya habari

Wiki chache baadaye alitangaza kwamba alikuwa tayari kukutana na wanachama wa Upinzani. Hatua hiyo ililenga kile alichosema kama kutaka kuleta 'uhuru wa kidemokrasia' nchini Tanzania

Hii ni kinyume na utawala wa Rais Magufuli , ambapo mtu yeyote aliyekosoa serikali angekabiliwa kisiasa na kuwekewa vikwazo

Baadhi ya wanachama wa upinzani waliunga mkono hatua hiyo , lakini wengine wamesema ni maneno matupu

Tangu tangazo hilo mnamo mwezi Mei, Rais Samia bado hajakutana na upinzani na kuangazia baadhi ya matakwa yao ikiwemo mabadiliko ya kikatiba

Rais Samia aliwavutia Wakenya wengi katika ziara yake ya siku mbili nchini humo

Kuimarisha uhusiano mwema

Rais Samia hadi sasa amefanya ziara tatu za kimataifa. Hii ni kwa nchi jirani Kenya na Uganda. Kisha mwishoni mwa mwezi Juni pia alitembelea Msumbiji.

Kenya na Tanzania zilikuwa na uhusiano uliogubikwa na mvutano wakati wa utawala wa rais Magufuli

Hii ilitokana na matukio ya kutisha yaliosababisha wasiwasi na hatua za kulipiza kisasi kati ya mataifa hayo mawili

Katika hotuba yake kwa bunge la kenya mwezi Mei, rais Samia alisisitiza kwamba uhusiano kati ya mataifa haya mawili haufai kuwa mbaya

Katika hotuba kwa bunge la Kenya mnamo mwezi Mei, rais Samia alisisitiza kwamba uhusiano kati ya mataifa hayo mawili haufai kuwa mbaya

Mataifa hayo mawili yaliahidi uhusiano mzuri wa kibiashara, ikiwemo kuondolewa kwa masharti na vikwazo vilivyowekwa

Mataifa hayo mawili yaliahidi uhusiano mzuri wa kibiashara, ikiwemo kuondolewa kwa masharti na vikwazo vilivyowekwa.

Tanzania kufikia sasa inavuna kutoka kwa ziara ya kiongozi wao nchini kenya mwezi Mei ambapo taifa hilo limeruhusu kuagiza mahindi kutoka kwa jirani yake.

Rais Samia akizindua matibabu katika Taasisi ya Jakaya Kikwete inayotibu magonjwa ya moyo.JKCI. IKULU YA RAIS TANZANIA

Akiangazia ushirikiano wa kiuchumi na na kupambana na uhalifu

Katika hotuba yake bungeni, rais Samia alisema kwamba serikali yake itakuza uwekezaji wa kimkakati , kurudisha imani ya wawekezaji na kuvutia uwekezaji wa kibinafsi.

Tangu wakati huo, ametia saini makubaliano ya dola milioni 3.5 na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhusu bomba la mafuta ghafi .

Hatua hiyo itaunda miundo msingi ya kuisaidia Uganda kusafirisha mafuta ghafi hadi katika masoko ya kimataifa.

Rais Samia pia aliagiza kuharakishwa kwa miradi ya pamoja na Rwanda , ikiwemo mradi wa umeme wa Rusumo.

Mradi wa Umeme wa Rusumo utazalisha umeme utakaotumika Tanzania, Burundi na Rwanda

Mnamo mwezi Machi, alimfuta kazi Mkurugenzi wa halmashauri ya bandari kutokana na madai ya ufujaji na kuanzisha uchunguzi kuhusu jinsi fedha zilivyotumika na Benki ya Tanzania

Hii inatokana na ripoti iliyofichua kwamba fedha za serikali zilitumiwa vibaya na baadhi ya Taasisi na uchunguzi kuanzishwa katika wizara ya fedha

Watanzania wamekuwa wakihoji ni lini matokeo ya uchunguzi huo yatatolewa kwa umma

Rais Samia anawasalimia watu katika ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo. IKULU YA RAIS TANZANIA

Kukabiliana na tatizo la kijinsia

Hatua ya Rais Samia kuingia katika siasa , imevunja kingo za ubaguzi wa kijinsia: Kutoka kuwa mwanake wa kwanza kuwa makamu wa Rais nchini Tanzania hadi kuwa Rais wa Kwanza mwanamke nchini humo

Mnamo mwezi Aprili, alichaguliwa kwa wingi wa kura kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , ambacho ndio chama kikubwa zaidi na kinachotawala nchini humo

Hatua hiyo inamfanya yeye kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhfa huo tangu CCM kuanzishwa mwaka 1977

Wakati wa uteuzi wa watawala wa mikoa mnamo mwezi Juni, aliahidi kwamba serikali yake itaheshimu usawa wa kijinsia katika uteuzi wa nyadhfa za serikali

Hatahivyo hakuzungumzia kuhusu matatizo ya kijinsia yalioangaziwa wakati wa utawala wa Rais Magufuli kama vile marufuku ya wasichana waliopatiwa ujauzito kutorudi shule

Badala yake , serikali yake imesema kwamba itaidhinisha elimu mbadala kwa wasichana wajawazito na kina mama wenye umri mdogo , ambayo ilikuwa imekubalika na serikali 2020

Walinzi wanawake wanaomlinda Rais Samia pia wamekuwa kivutio cha wengi nje na ndani ya Tanzania. Wengi wamepongeza hatua hiyo kama endelevu inapokuja suala la uwakilishaji katika sekta iliyotawaliwa na wanaume

Itifaki za serikali ya Tanzania inasema kwamba ni vyema kwa Rais wa kike kuwa na walinzi wanawake, iwapo rais anataka iwe hivyo

Hi ni tabia ambayo amekuwa nayo tangu siku zake kama makamu wa Rais