1. Daktari wa upasuaji wa ubongo
2. Daktari wa tiba ya kiasili
3. Muuzaji dhahabu
1. Kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama
2. Kuimarisha uhusiano wa Uingereza na bara Afrika.
3. Kuimarisha sekta ya utalii barani Afrika.
1. Neymar
2. Lionel Messi
3. Zlatan Ibrahimovic
1. Kufikia 2020
2. Kufikia 2023
Kufikia 2030
1. Saa 2 Dakika 2 Sekunde 57
2. Saa 2 Dakika 1 Sekunde 30
3. Saa 2, Dakika 1 na Sekunde 39
1. Begi
2. Mkongojo
3. Suti
1. Mali
2. Afrika Kusini
3. Ghana
Sahihi: Daktari wa tiba ya kiasili
Dkt Anthony Mwandulami ni daktari wa tiba ya kiasili na lengo lake ni kuihifadhi historia yake
baada ya kifo.
Mwandulami anasema ndani ya kaburi hili, atazikwa yeye pamoja na wake zake watatu.
Amechimba chini mita 12 na amesema mwili wake utakaushwa kabla ya kuhifadhiwa.
https://www.bbc.com/swahili/habari-45584179
Sahihi: Kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama
Mwanamfalme William wa Uingereza ataruzu Afrika kwa lengo la kukabiliana na ujangili na uhifadhi
wa wanyama.
William ni rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk
Trust.
Anatarajiwa kuzuru Tanzania, Kenya na Namibia.
Usikose kupata habari za mwanamfalme Harry kwenye
Sahihi: Zlatan Ibrahimovic
Mshambuliaji wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic, amejiunga na wachezaji ambao wamefunga magoli 500 na
zaidi wakichezea timu kubwa ya klabu na taifa.
Ibrahimovic, alifunga bao la kushangaza dhidi ya Toronto nchini Marekani.
Messi tayari ni miongoni mwa wachezaji ambao wamefunga magoli 500 kwa hivi sasa amefunga magoli
365 katika mechi zote.
Sahihi: Kufikia 2023
Bilionea wa Kijapani Yusaku Maezawa,42, anatarajiwa kusafiri mwezi kufikia mwaka 2023 pamoja na
kundi la wasanii.
Maezawa,hajafahamu bado ni kiasi gani cha fedha anapaswa kukilipa kwa safari hiyo ambayo
itawaunganisha pamoja na mabilionea wengine wawili ambao hawajulikani sana duniani.
Mjapani huyo alianza kama mjasiriamali wa kuuza CD ambazo zilikuwa adimu.
Sahihi: Saa 2, Dakika 1 na Sekunde 39
Bingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge alitumia muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 39.
Kipchoge, mwenye umri wa miaka 33, ameshinda mara kumi kati ya marathon 11 alizokimbia.
Kipchoge kwa sasa ndiye anayeshikilia rekodi mpya ya mbio za marathon duniani.
Sahihi: Begi
Bobi alipowasili Uganda kutoka Marekani, alikokuwa amekwenda kupokea matibabu alikuwa na begi
nembo ya bidhaa za kifahari - Luis Vuitton.
Alikuwa na mkongojo lakini haukuzua mjadala miongoni mwa wakosoaji wake.
https://www.bbc.com/swahili/habari-45588883
Sahihi: Afrika kusini
Afrika kusini
Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini imehalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika
maeneo faragha.
Mwezi Aprili Zimbabwe ilikuwa nchi ya pili barani Afrika baada ya Lesotho kuhalalisha bangi kwa
matumizi ya kiafya.
https://www.bbc.com/swahili/habari-45570162